Swali: Kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua baada ya Rukuu´ ni Sunnah au Bid´ah? Ni ipi dalili?
Jibu: Maoni sahihi katika hilo ni kwamba ni Sunnah kutokana na Hadiyth ya Sahl bin Sa´d, na ipo katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy, ambaye amesema:
“Watu walikuwa wakiamrishwa mtu kuweka mkono wake wa kuume juu ya dhiraa yake ya kushoto ndani ya swalah.”
Hadiyth hii ni yenye kuenea. Vilevile maneno yake:
“… ndani ya swalah.”
ni yenye kuenea katika hali zake zote isipokuwa yale ambayo yamevuliwa na dalili. Muulizaji awe pamoja nasi ili tutazame kuinuka kutoka katika Rukuu´ kunaingia ndani ya Hadiyth hii au hakuingii. Sisi tunasema kwamba maneno yake:
“… ndani ya swalah.”
ni yenye kuenea. Kunaingia kwanza hali ya kusimama kabla ya kwenda katika Rukuu´. Hali ya Rukuu´ haingii kwa sababu kunapowekwa mikono katika Rukuu´ kunatambulika; ni kwamba inawekwa kwenye magoti mawili. Tunaangalizia kuinuka kutoka katika Rukuu´ kwa sababu ndio swali lililoulizwa. Hali ya Sujuud haiingii kwa sababu kunapowekwa mikono katika Sujuud kunatambulika; inawekwa ardhini. Wala hali ya kikao kati ya Sujuud mbili haiingii kwa sababu inapowekwa mikono baina ya Sujuud mbili kunajulikana ni wapi; inawekwa juu ya mapaja. Wala hali ya kikao katika Tashahhud ya kwanza na Tashahhud ya pili haiingii kwa sababu inapowekwa mikono miwili kunajulikana ni wapi; ni juu ya mapaja. Imebaki hali ya kuinuka kutoka katika Rukuu´; tunasema kuwa kuinuka kutoka katika Rukuu´ ueneaji wa Hadiyth ya Sahl hii inaikusanya hukumu ya mikono miwili baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´. Kujengea juu ya hili hukumu ya mikono miwili baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´ hukumu yake ni sawa na kabla ya Rukuu´. Bi maana mkono wa kulia utawekwa juu ya mkono wa kushoto.
Kuhusu ambaye amesema kuwa ni Bid´ah[1]; bi maana kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´ hakuzingatia Hadiyth hii. Angeizingatia basi angelibainikiwa na jambo kama tulivyoweka wazi.
Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) imepokelewa kwamba ametoa khiyari kati ya mtu kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´ na kati ya kuiachia. Huenda (Rahimahu Allaah) hakubainikiwa na hukumu katika masuala haya na ndio maana akafanya ni jambo la khiyari. Au pengine ameziona Hadiyth zengine mbali na Hadiyth ya Sahl zinazofahamisha juu ya kuiachia na hivyo ndio maana akafanya ni jambo la khiyari. Kwa sababu jambo linalotakikana kwa mwanafunzi ni asipopata dalili juu ya masuala fulani basi ajizuie na wala asitoe khiyari. Kwani kufutu juu ya kutoa khiyari ni hukumu. Haijuzu kutoa hukumu isipokuwa kwa dalili. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) hawezi kuhukumu utoaji khiyari isipokuwa atakuwa na dalili juu ya hilo.
Muhimu ni kwamba kusema kuwa kitendo hicho ni Bid´ah – yaani kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´ kwamba ni Bid´ah – ni maoni yasiyokuwa na mashiko. Bali maoni ya sawa yanayofahamishwa na Hadiyth ya Sahl ni kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´. Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] Tazama https://firqatunnajia.com/al-albaaniy-kuhusu-mahali-pa-mikono-baada-ya-rukuu/
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (62) http://binothaimeen.net/content/13449
- Imechapishwa: 10/01/2020

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (62) http://binothaimeen.net/content/13449
Imechapishwa: 10/01/2020
https://firqatunnajia.com/ibn-uthaymiyn-kuhusu-mahali-pa-mikono-baada-ya-rukuu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)