Swali: Baadhi ya watu wanatofautiana juu ya kuangalia maigizo mashuleni na kwenginepo. Unasemaje? Je, inafaa kugombana na kukatana kwa sababu ya tofauti kama hizi?

Jibu: Kuhusu sehemu ya mwisho ya swali, haijuzu. Haijuzu kuzozana na kukatana kwa sababu ya tofauti hii. Hakuna dalili inayoharamisha wala kuhalalisha. Ni jambo ambalo wanazuoni wamelifanyia Ijtihaad. Kwa hivyo haijuzu kugombana na kususana kwa sababu yake. Kuhusu hukumu yake, hakika nimelibainisha katika “Majmuu´-ur-Rasaa-il wal-Masaa-iyl”. Rejea huko, kwani swali linahitajia upambanuzi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (159 B)
  • Imechapishwa: 21/09/2021