Ibn ´Uthaymiyn anafunga mlango wa utumiaji mbaya wa Takfiyr

Swali: Ni ipi hukumu juu ya mtawala anayehukumu kwa kitu ambacho hakukiteremsha Allaah licha ya kwamba anaamini ndani ya moyo wake kuwa ni lazima kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah?

Jibu: Masuala haya sio mepesi. Wala hayawezi kutolewa hukumu yenye kuenea. Kwa sababu ikiwa kutatolewa hukumu kwa njia yenye kuenea, baadhi ya watu watafahamu kimakosa. Mtawala akifanya kitu ambacho mtu huyu yeye anaonelea kuwa ni Shari´ah ya Allaah, basi atasema kuwa ni kafiri. Ni kama ambavo hali ilivo hii leo baadhi ya makundi yanawakufurisha watawala kwa sababu wanaona kuwa amehukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah licha ya kwamba hawakuyafahamu vizuri wala kuyasoma masuala haya.

Kwa ajili hiyo mimi naona kuwa bora zaidi ni kufunga mlango juu ya masuala haya ili watu wasije kufahamu kimakosa kinyume na alivokusudia mtoa fatwa na wasije kuyatumia kama njia ya kuwafanyia uasi watawala wa nchi zao.

Wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wameyazungumzia masuala haya katika mnasaba wa zile Aayah zilizomo katika Suurah al-Maaidah. Unaweza kurejea huko juu ya yale yaliyosemwa na wanachuoni juu ya masuala hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa´ al-Baab al-Maftuuh (78 A)
  • Imechapishwa: 20/12/2020