al-Haakim amesema: Nimemsikia Abu Sa´iyd ´Abdur-Rahmaan bin Ahmad al-Muqriy akisema: Nimemsikia Abu Bakr Muhammad bin Ishaaq akisema:

”Nasema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah ambayo hayakuumbwa, wahy na yameteremshwa. Mwenye kusema kuwa Qur-aan ni kitu au kitu katika hiyo au Wahy Wake au ushukaji Wake umeumbwa, au kwamba Allaah hazungumzi tena baada ya kuitamka milele, au kwamba matendo ya Allaah yameumbwa, au kwamba Qur-aan ni kitu kilichozuka (حديث), au kwamba kitu katika sifa za Allaah (sifa za kidhati) au kitu katika majina ya Allaah kimeumbwa, naonelea kuwa ni Jahmiy. Anatakiwa kuambiwa kutubia. Akitubia ni sawa na la sivyo akatwe shingo yake na atupwe sehemu ya taka. Hii ndio ´Aqiydah nilionayo na ´Aqiydah walionayo wanachuoni mashariki na magharibi. Mwenye kuonelea kinyume ni mwongo na mzushi. Yule mwenye kusoma vitabu vyangu ya kielimu ataona kuwa Kullaabiyyah – Allaah awalaani – wananisemea uongo na ´Aqiydah yangu. Watu wote mashariki na magharibi wanajua kuwa hakuna ambaye ameandika vitabu vya kielimu kuhusu Tawhiyd, Qadar na misingi kama nilivyofanya. Mwenye kusema kitu kingine mbali na yale yaliyomo ndani ya vitabu vyangu ni mwongo na mzushi.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (6/171)
  • Imechapishwa: 27/03/2019