Ibn Baaz Twawaaf wakati wa Khutbah II

Swali 429: Vipi kuhusu kufanya Twawaaf wakati wa Khutbah?

Jibu: Aikatishe Twawaaf, kisha asikilize Khutbah.

430 – Kisha Shaykh akaulizwa kuhusu anayetufu na hana swalah ya ijumaa?

Jibu: Pengine ikasemwa kwamba anawasumbua waliopo pale. Kikosi cha wanzuoni wamesema kuwa msafiri akikutwa na swalah ya ijumaa basi inamlazimu. Katika hali hiyo anyamaze na atufu baada ya swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 140
  • Imechapishwa: 28/08/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´