Ibn Baaz shirki ndogo inasamehewa au haisamehewi?

Swali: Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.” (an-Nisaa´ 04:48)

Je, ndani yake kunaingia shirki kubwa na ndogo au kubwa peke yake?

Jibu: Maoni yaliyo karibu na usawa ni kwamba shirki ndogo haikusudiwi. Inaweza kusamehewa kwa sababu mizani ya matendo mema ni yenye nguvu zaidi. Kwa sababu ni aina moja wapo ya madhambi makubwa. Lakini huenda mtu asisamehewe ikiwa hatoomba msamaha na mizani yake isiwe na uzito. Katika hali hii huenda akaadhibiwa kwayo. Kama mfano wa mwenye kuadhibiwa kwa sababu ya madhambi makubwa ikiwa mtu atakufa juu yake. Isipokuwa ikiwa kama Allaah atamsamehe.

Swali: Kwa hiyo msingi ni kwamba shirki ndogo ni dhambi kubwa zaidi kuliko madhambi makubwa?

Jibu: Haya ndio maoni yaliyo karibu zaidi na usawa na yaliyo dhahiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 28
  • Imechapishwa: 23/03/2019