Swali: Mtu ana deni kwa sarafu ya kimisri. Je, inajuzu kulilipa kwa sarafu isiyo ya kimisri?
Jibu: Ndio, wakikubaliana juu ya hilo hapana ubaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa:
”Ee Mtume wa Allaah! Tunauza kwa dirhamu kisha tunachukua dinari, na tunauza kwa dinari kisha tunachukua dirhamu.” Akasema: ”Hapana vibaya kuchukua kwa thamani ya siku hiyo mpaka muachane na kati yenu hakuna kitu.”
Kwa hiyo ikiwa ameuza kwa sarafu ya kimisri kisha akachukua badala yake kwa sarafu ya kisaudi au nyingine mkono kwa mkono, papohapo katika kikao, hapana vibaya kwa masharti ya kubadilishana kwa wakati huo katika kikao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30934/هل-يجوز-قضاء-الدين-بعملة-مختلفة
- Imechapishwa: 13/09/2025
Swali: Mtu ana deni kwa sarafu ya kimisri. Je, inajuzu kulilipa kwa sarafu isiyo ya kimisri?
Jibu: Ndio, wakikubaliana juu ya hilo hapana ubaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa:
”Ee Mtume wa Allaah! Tunauza kwa dirhamu kisha tunachukua dinari, na tunauza kwa dinari kisha tunachukua dirhamu.” Akasema: ”Hapana vibaya kuchukua kwa thamani ya siku hiyo mpaka muachane na kati yenu hakuna kitu.”
Kwa hiyo ikiwa ameuza kwa sarafu ya kimisri kisha akachukua badala yake kwa sarafu ya kisaudi au nyingine mkono kwa mkono, papohapo katika kikao, hapana vibaya kwa masharti ya kubadilishana kwa wakati huo katika kikao.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30934/هل-يجوز-قضاء-الدين-بعملة-مختلفة
Imechapishwa: 13/09/2025
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kulipa-deni-kwa-pesa-nyingine-02/