Swali: Je, mwalimu anayewafundisha watoto anapaswa kuwaamuru kutawadha?

Jibu: Ikiwa watoto wamefikia umri wa miaka saba, basi awaamrishe kutawadha. Lakini watoto walio chini ya umri wa miaka saba, mwalimu awaandikie mahitaji yao kwenye karatasi au ubao.

Swali: Afanye hivi muda wa kuwa hajawafikisha miaka ya kuwawajibikia ´ibaadah?

Jibu: Asiwaache kushika msahafu. Awaandikie nayo mahali pengine, kwa sababu wako katika mwaka wa kwanza. Miaka saba ni katika mwaka wa kwanza kama mwanafunzi.

Swali: Hata kama Qur-aan hiyo ni majuzu?

Jibu: Awaandikie nayo kwenye karatasi. Kufanya hivo ni sahali zaidi kuliko kuwapa msahafu au acheleweshe kuwafunza Qur-aan mpaka wafikishe miaka saba ili apate kuwafunza kwanza twahara.

Swali: Je, makinzano ni kuhusiana na watoto waliofikisha miaka ya kuweza kupambanua mambo au wale waliobaleghe?

Jibu: Tofauti ni kuhusu watoto waliofikisha miaka ya kuweza kupambanua mambo na waliokishabaleghe. Watoto waliofikisha miaka ya kuweza kupambanua mambo wanapaswa kufunzwa twahara na waliokwishabaleghe jambo lao linatambulika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24746/هل-يومر-الاطفال-بالوضوء-لتعلم-القران
  • Imechapishwa: 08/12/2024