Ibn Baaz kuhusu wanawake kucheza harusini

Swali: Ni ipi hukumu ya kucheza michezo kwenye harusi, kama vile kucheza bila ngoma au shughuli kama hizo?

Jibu: Ndoa inatakiwa itangazwe kwa kutumia dufu na nyimbo zilizozoeleka miongoni mwa wanawake wakati wa usiku. Hili ni katika kutangaza ndoa ili isitafsiriwe kuwa ni uzinifu. Wanawake wanaporuhusiwa kuimba miongoni mwao kwa nyimbo zao za kawaida za kumsifu mume au watu wa upande wa bibi harusi na mfano wa hayo au kupiga dufu baina yao bila kuchanganyika na wanaume, basi hakuna ubaya katika hilo. Kucheza, ikiwa mwanamke anacheza kati ya wanawake wenzake, kama dada zake, basi hapana vibaya. Ama “khatwah”, hatuijui maana yake. Ikiwa maana yake ni kucheza kati ya wanawake au kuandaa chakula kwa ajili ya jamaa, basi hilo pia halina ubaya. Inafaa kwa muulizaji kufafanua maana ya “khatwah” ni nini na sifa yake ni ipi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/40)
  • Imechapishwa: 18/03/2026