Swali: Je, mtu anakufurishwa akiomba kinga kutoka kwa kaburi la mtu mwema hali ya kuwa ni mjinga?
Jibu: Ndio, ni shirki kubwa. Haya ni miongoni mwa yale mambo ambayo hayajifichi kati ya waislamu.
Swali: Je, anakufuru akiwa ni mjinga?
Jibu: Haijalishi kitu. Haya ni miongoni mwa ukafiri mkubwa na wala hapewi udhuru kwa kusema eti ni mjinga. Ni jambo ambalo linatambulika fika katika dini. Hata hivyo akiwa ni mkweli basi aharakishe kutubia.
Swali: Katika baadhi ya miji wanayazunguka?
Jibu: Ndio, Shaam, Misri na kwingineko.
Swali: Je, wanakufuru?
Jibu: Ndio, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakufurisha na waislamu wakawapiga vita. Waliwapiga vita wanakuzimu na miongoni mwao wako watu wajinga wasiojua kitu ambao wanaingia kwenye mkumbo mmoja wa mabwana zao.
Swali: Uchinjaji?
Jibu: Kuchinja kwa asiyekuwa Allaah ni shirki:
قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ
“Sema: “Hakika swalah yangu, kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.”[1]
Swali: Katika nchi maalum?
Jibu: Wajinga wanaingia kwenye mkumbo mmoja wa viongozi wao. Wanaungana na makafiri. Wanaingia kwenye mkumbo wa mayahudi, manaswara na mfano wao. Wanawafata viongozi wao. Wajinga wao wanawafata.
[1] 06:162-163
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24589/حكم-من-استغاث-بقبر-احد-الصالحين-جاهلا
- Imechapishwa: 11/11/2024
Swali: Je, mtu anakufurishwa akiomba kinga kutoka kwa kaburi la mtu mwema hali ya kuwa ni mjinga?
Jibu: Ndio, ni shirki kubwa. Haya ni miongoni mwa yale mambo ambayo hayajifichi kati ya waislamu.
Swali: Je, anakufuru akiwa ni mjinga?
Jibu: Haijalishi kitu. Haya ni miongoni mwa ukafiri mkubwa na wala hapewi udhuru kwa kusema eti ni mjinga. Ni jambo ambalo linatambulika fika katika dini. Hata hivyo akiwa ni mkweli basi aharakishe kutubia.
Swali: Katika baadhi ya miji wanayazunguka?
Jibu: Ndio, Shaam, Misri na kwingineko.
Swali: Je, wanakufuru?
Jibu: Ndio, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakufurisha na waislamu wakawapiga vita. Waliwapiga vita wanakuzimu na miongoni mwao wako watu wajinga wasiojua kitu ambao wanaingia kwenye mkumbo mmoja wa mabwana zao.
Swali: Uchinjaji?
Jibu: Kuchinja kwa asiyekuwa Allaah ni shirki:
قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ
“Sema: “Hakika swalah yangu, kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.”[1]
Swali: Katika nchi maalum?
Jibu: Wajinga wanaingia kwenye mkumbo mmoja wa viongozi wao. Wanaungana na makafiri. Wanaingia kwenye mkumbo wa mayahudi, manaswara na mfano wao. Wanawafata viongozi wao. Wajinga wao wanawafata.
[1] 06:162-163
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24589/حكم-من-استغاث-بقبر-احد-الصالحين-جاهلا
Imechapishwa: 11/11/2024
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-wajinga-wanaojilinda-na-wafu/