Ibn Baaz kuhusu salamu za kubusu mikono

Swali: Ni ipi hukumu ya kubusu mkono?

Jibu: Bora ni kuacha kufanya hivo.

Swali: Yaliyofanywa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Baadhi ya watu waliweza kufanya hivo kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baadhi ya maimamu wametilia hilo mkazo. Hata hivyo bora ni kuacha kufanya hivo. Baadhi ya wanazuoni wanaita kuwa ni aina ndogo ya sujudu. Kwa hiyo bora ni kuacha hivo. Haitakiwi kutilia mkazo wala kuchukulia wepesi. Bora ni kuacha kufanya hivo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24578/ما-حكم-تقبيل-اليد
  • Imechapishwa: 03/11/2024