Swali: Shaykh mtukufu, Allaah Akujaze kheri. Mwandishi wa kitabu “Manhaj-ul-Anbiyaa fid-Da’wah ilaa Allaah” amesema:

“Nimesoma vitabu vya ´Aqiydah na kupata kuona kuwa vinachosha kwa sababu vina maandiko na hukumu (Nusuus na Ahkaam).”

Unasemaje kuhusu hili?

Jibu: Hilo ni kosa kubwa kabisa. Vyote vinachosha? Ninaomba kinga kwa Allaah. Vitabu vya ‘Aqiydah sahihi havichoshi kabisa. Kwa sababu vina maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa anaelezea Qur-aaan na Sunnah kuwa vinachosha, inazingatiwa kuwa ni kuritadi (Riddah) kutoka katika Uislamu – tunaomba Allaah Atusamehe. Kinachochosha ni kuipa mgongo Dini ya Allaah na sio kufanyia kazi Shari´ah. Hilo linachosha! Kuandika kuhusu ´Aqiydah na kulingania katika ´Aqiydah sahihi ambayo walikuwemo Salaf-us-Swaalih sio jambo linalochosha. Kwa sababu hii ndio Dini ya Mitume. Ni mfumo huo ndio ambao Mitume walishikamana nao wakati walipokuwa wakilingania katika Dini ya Allaah. Walibainisha ´Aqiydah sahihi na wakatahadharisha yale yanayokwenda kinyume nayo. Maneno haya ni ya kigonjwa na jarima.

Swali: Ni yapi maoni yako kuhusu kuuza kitabu hichi?

Jibu: Ikiwa kina haya, haijuzu kukiuza. Ni lazima kukichana ikiwa maneno haya yamo humo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda ”Ma´ Mashâyikh ad-Da´wah as-Salafiyyah”, sehemu ya 2
  • Imechapishwa: 22/04/2015