Ibn Baaz kuhusu midoli ya watoto yenye picha za viumbe wenye roho

Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu kuhusu midoli ya watoto? Je, inajuzu kwa sababu wao ni watoto hata kama ni ya sura ya viumbe?

Jibu: Kuna tofauti ya maono miongoni mwa wanazuoni kuhusu hilo. Miongoni mwa hoja zinazotolewa ni Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa):

“Alikuwa na wanasesere wadogo.”

Baadhi ya wanazuoni wanasema inasameheka kwa sababu ni vitu vinavyodharauliwa. Lakini wanazuoni wengine wamepinga, wale waliokuwa kwa ‘Aaishah hawakuwa picha za viumbe zenye roho kama tunavyojua leo, bali vilikuwa ni vitu vya kawaida ambavyo waarabu walikuwa wanavitengeza – wanashona nguo au vitambaa na kuviwekea vijiti, havikuwa na sura kamili. Basi tahadhari zaidi ni kuacha kuvitumia kutokana na Hadiyth nyingi ambazo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amewalaani wapiga picha na akasema:

“Hakika wao ndio watu wenye adhabu kali zaidi siku ya Qiyaamah.”

Amesema kumwambia ‘Aliy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

“Usiache picha yoyote isipokuwa umeifuta.”

Hivyo Hadiyth hizi ni zenye kuenea.

Na yale aliyokuwa nayo ‘Aaishah yanaweza kubeba maana kuwa hayakuwa picha kama hizi zinazochorwa au kutengenezwa kwa maumbo ya leo, bali vilikuwa ni vitambaa vilivyowekwa kwenye vijiti kana kwamba ni midoli.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28498/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%88%D8%B1%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%88%D8%AC%D9%87-%D9%81%D9%8A%C2%A0%D9%84%D8%B9%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B7%D9%81%D8%A7%D9%84
  • Imechapishwa: 21/04/2025