Swali: Hadiyth si yenye kufasiri wivu wa Allaah…

Jibu: Maana yake ni kumkaripia na kuchukia kitendo chake. Wivu wa Allaah ni sifa ya Allaah maalum inayolingana Naye tu na haifanani na sifa za viumbe. Ni kule kumkaripia Kwake mja anapofanya yale Aliyoharamisha, kukichukia kitendo Chake na kumkataza Kwake. Vivyo hivyo kuhusu bughudha Yake, makaripio na makatazo. Yote haya yanapelekea kuwakataza watu kutokana na mambo hayo.

Swali: an-Nawawiy hakuzidisha juu ya hayo?

Jibu: Wivu ni sifa maalum.

Swali: Amefasiri wivu kwa maneno yake katika Hadiyth…

Jibu: Anachokusudia ni kwamba wivu ni makatazo, lakini wivu sio makatazo. Wivu unapelekea kwenye makatazo. Wivu wa Allaah ni sifa ya Allaah inayolingana na Allaah pekee. Wivu maana yake ni kubughudhi na kuchukia. Imekaribia maana hiyo na sio kukataza. Ni kule kukaripia na sio kukataza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24469/معنى-وغيرة-الله-ان-ياتي-المومن-ما-حرم-عليه
  • Imechapishwa: 22/10/2024