Swali: Je, inafaa kuswali nyuma ya mtu ambaye ana ´Aqiydah inayokwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kama mfano wa Ashaa´irah?
Jibu: Maoni ya sawa – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba kila ambaye tunamuhukumu kuwa ni muislamu basi inasihi kuswali nyuma yake. Vinginevyo itakuwa haifai. Haya ndio maoni ya jopo la wanachuoni na ndio maoni ya sawa.
Ambaye amesema kuwa haijuzu kuswali nyuma ya mtenda dhambi maoni yake ni dhaifu. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameruhusu kuswali nyuma ya watawala. Kama inavotambulika watawala wengi ni watenda madhambi. Ibn ´Umar, Anas na kikosi cha Maswahabah wengine waliswali nyuma ya al-Hajjaaj ambaye ni miongoni mwa watu madhalimu kabisa.
Kwa kifupisha ni kwamba swalah inasihi nyuma ya mzushi ambaye ana Bid´ah zisizomtoa nje ya Uislamu au mtenda dhambi mwenye dhambi zisizomtoa nje ya Uislamu. Lakini hata hivyo inapaswa kumteua mtu wa Sunnah. Vivyo hivyo watu wakikusanyika wanapaswa kumtanguliza mbele yule ambaye ni mbora wao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/426)
- Imechapishwa: 31/01/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
38. Swalah ya ijumaa nyuma ya watawala
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema: “Swalah ya ijumaa nyuma yao na nyuma ya magavana wao inafaa na ni timilifu na ni Rak´ah mbili. Yule mwenye kuirudi ni mtu wa Bid´ah mwenye kuyaacha mapokezi na anaenda kinyume na Sunnah. Hapati chochote katika fadhila za ijumaa midhali haonelei kuwa ni…
In "Itmaam-ul-Minnah"
Ahl-ul-Bid´ah ndio hawaswali nyuma ya mtenda dhambi
Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema: "Tunaona kuswali nyuma ya kila ambaye ni mwema au muovu miongoni mwa waislamu." Kuswali nyuma ya kila ambaye ni mwema au muovu ni miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Tofauti na Ahl-ul-Bid´ah. Tofauti na Ahl-ul-Bid´ah hawaswali nyuma ya viongozi madhalimu wala nyuma ya mtenda dhambi.…
In "ar-Raajihiy kuhusu Mu´tazilah"
Wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah kuhusu kuswali nyuma ya mtenda dhambi
Ikiwa sio mtawala ndiye mwenye kuongoza Ijumaa na idi, bali ni imamu aliyeteuliwa na nchi au kukawa hakuna imamu mwingine na huyu aliyewekwa ni mtenda dhambi, kunaswaliwa nyuma yake au hakuswaliwi? Jibu ni kwamba kunaswaliwa nyuma ya mtenda dhambi katika hali mbili: 1 - Ikiwa huyu ndiye mtawala wa waislamu…
In "Msimamo juu ya makosa ya imamu"