Ibn Baaz kuhusu kumuomba mtu mwingine akuombee du´aa

Swali: Maneno yake Shaykh-ul-Islaam ya kwamba bora ni kuacha kumuomba ndugu yako akuombee du´aa?

Jibu: Kinachodhihiri ni kwamba maneno yake Shaykh-ul-Islaam katika hili hayana nguvu. Sunnah ni yenye kutangulizwa mbele yake na mbele ya wengine. Sunnah inatamka wazi juu ya hili. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

”Akimuombea du´aa ndugu yake Malaika aliyewakilishwa husema: ”Nawe upewe hayohayo.”

Ni jambo linaloleta shauku juu ya hili. Hadiyth iko wazi na ni Swahiyh kaipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake. Hadiyth ya ´Umar iko wazi, ijapo imezungumziwa, hata hivyo kuna ambazo zinaitia nguvu inapokuja katika maana. Ni kumfanyia wema nduguyo.

Lakini baadhi ya watu wanapindukia katika jambo hili, jambo ambali hawatakiwi kulifanya. Kila unapokutana naye na akakuona anakwambia:

”Usinisahau katika du´aa yako.”

Kila saa. Bora ni kuacha kufanya hivo. Ni sawa kumuomba akuombee du´aa katika baadhi ya nyakati na isiwe kwa kukariri. Usimng´ang´anie daima, kwa sababu jambo hilo linaweza kuwa vigumu kwa watu. Hata hivyo ni sawa ikiwa mtu anafanya hivo baadhi ya nyakati, muda mrefu hamuonani na mfano wake. Pengine ikawa ni bora kufanya hivo kuliko kukithirisha.

Swali: Mtu amwombe ndugu yake du´aa anaposafiri kwa sababu ameahidiwa kujibiwa?

Jibu: Muhimu ni kwamba mtu asifanye hivo kwa wingi, kwa sababu kukithirisha kunaweza kuudhi na kuwatia uzito watu.

Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”… kisha mniombee wasiylah na fadhilah… ”

ndani yake si kuna dalili ya kuomba du´aa kutoka kwa mtu aliye chini?

Jibu: Namna hiyo. Hilo liko mahali pake kabisa, umefanya vizuri. Amefanya hivo ilihali yeye ndiye mbora wa viumbe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24461/هل-طلب-الدعاء-من-الغير-افضل-ام-تركه
  • Imechapishwa: 16/10/2024