´Allaamah ar-Raajihiy: Vipi kuhusu maneno yake:

”Hana [mkono wa] kushoto Muumba wetu.”?

Jibu: Kuna makinzano katika jambo hili. Sahihi ni kwamba umethibiti, kama ilivyokuja katika Hadiyth ya Ibn ´Umar:

”Anashika mbingu kwa mkono Wake wa kulia na ardhi kwa mkono Wake wa kushoto.”

Ingawa ndani yake kuna unyonge, kwa sababu ni katika mapokezi ya baadhi ya watoto wa ´Umar na ndani yake kuna udhaifu. Lakini riwaya nyingine zinaunga mkono. Kwa kuwa kuuita mmoja wao kuwa ni wa kulia, kunamaanisha kuwa mwingine umeitwa kushoto. Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mikono yote miwili ya Mola wangu ni ya kulia yenye baraka.”

Yote ni ya kulia inapokuja katika ubora na utukufu, hata kama wa pili utaitwa wa kushoto, lakini kwa heshima ni wa kulia. Mikono yote ya Mola wangu ni ya kulia yenye baraka, kama ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh:

“Waadilifu watakuwa juu ya mimbari za nuru upande wa mkono wa kulia wa Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall) na mikono Yake yote ni ya kuume na yenye baraka; ni wale wanaofanya uadilifu katika hukumu zao, familia zao na yale wanayoyasimamia.”[1]

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume.”[2]

Hadiyth imetaja kwamba ataikamata ardhi kwa mkono Wake wa kushoto.

´Allaamah ar-Raajihiy: Mtunzi amesema kwa sababu mkono wa kushoto ni katika sifa za viumbe?

Ibn Baaz: Huenda Hadiyth ilifichikana (Rahimahu Allaah). Hakuitolea maelezo yoyote?

´Allaamah ar-Raajihiy: Hapana.

[1] Muslim (1827).

[2] 39:67

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31081/ما-حكم-نفي-الشمال-عن-المولى-جل-وعلا
  • Imechapishwa: 01/10/2025