Swali: Maneno yake aliposema kuwa Allaah ni wa kale?
Jibu: Sijui kwamba kumepokelewa jambo lolote juu yake katika Hadiyth Swahiyh, japokuwa baadhi ya watu hulitumia. Hata hivyo maana yake ni sahihi. Maana ya ukale ambao kabla yake hapakuwa na uhai wowote, kwa maana ya kwamba Yeye ndiye wa mwanzo. Jina la wa Mwanzo ndilo lililokuja katika dalili. Naye (Subhaanah) hakutanguliwa na chochote. Yeye ndiye wa Mwanzo kabla ya kila kitu. Kwa ajili hii halikupokelewa katika majina Yake (Subhaanah). Allaah amesema:
وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ
“Mwezi Tumeukadiria vituo mpaka ukarudi mwembamba kama karara kongwe.”[1]
Ameuita wa kale. Kuhusu majina Yake imekuja ya kwamba Yeye ni wa Mwanzo, kwa sababu hakuna chochote kinachomfanana Naye (Subhaanah).
Swali: Lakini vipi maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
أعوذ بالله العظيم وبوجهه الكريم وسلطانه القديم
”Najikinga kwa Allaah Aliyetukuka, kwa uso Wake mtukufu na kwa mamlaka Yake ya kale?”
Jibu: Hii ni sifa ya mamlaka.
´Allaamah ar-Raajihiy: Ameifungamanisha kwa kusema:
”Allaah ni wa kale wa milele.”?
Ibn Baaz: Ndio.
´Allaamah ar-Raajihiy: Je, hili linakuwa katika mlango wa taarifa?
Ibn Baaz: Hili linakanusha kile kinachoweza kudhaniwa.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu Mwenye kubaki limethibiti?
Ibn Baaz: Silitambui.
´Allaamah ar-Raajihiy: Je, lengo la mtunzi linakuwa kwamba anatoa taarifa juu ya Allaah kwa hili?
Jibu: Majina ya Allaah ni kwa mujibu wa dalili ya Qur-aan na Sunnah tu. Hayathibitiki isipokuwa kwa yale yaliyokuja katika Maandiko. Lakini maana yake ni sahihi. Yeye ndiye Aliyebaki daima. Maana yake ni sahihi. Yeye ndiye Aliyebaki daima. Lakini haisemwi kuwa ni miongoni mwa majina Yake ispokuwa kwa kuwepo dalili.
[1] 36:39
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31070/ما-حكم-قول-ان-الله-قديم
- Imechapishwa: 01/10/2025
Swali: Maneno yake aliposema kuwa Allaah ni wa kale?
Jibu: Sijui kwamba kumepokelewa jambo lolote juu yake katika Hadiyth Swahiyh, japokuwa baadhi ya watu hulitumia. Hata hivyo maana yake ni sahihi. Maana ya ukale ambao kabla yake hapakuwa na uhai wowote, kwa maana ya kwamba Yeye ndiye wa mwanzo. Jina la wa Mwanzo ndilo lililokuja katika dalili. Naye (Subhaanah) hakutanguliwa na chochote. Yeye ndiye wa Mwanzo kabla ya kila kitu. Kwa ajili hii halikupokelewa katika majina Yake (Subhaanah). Allaah amesema:
وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ
“Mwezi Tumeukadiria vituo mpaka ukarudi mwembamba kama karara kongwe.”[1]
Ameuita wa kale. Kuhusu majina Yake imekuja ya kwamba Yeye ni wa Mwanzo, kwa sababu hakuna chochote kinachomfanana Naye (Subhaanah).
Swali: Lakini vipi maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
أعوذ بالله العظيم وبوجهه الكريم وسلطانه القديم
”Najikinga kwa Allaah Aliyetukuka, kwa uso Wake mtukufu na kwa mamlaka Yake ya kale?”
Jibu: Hii ni sifa ya mamlaka.
´Allaamah ar-Raajihiy: Ameifungamanisha kwa kusema:
”Allaah ni wa kale wa milele.”?
Ibn Baaz: Ndio.
´Allaamah ar-Raajihiy: Je, hili linakuwa katika mlango wa taarifa?
Ibn Baaz: Hili linakanusha kile kinachoweza kudhaniwa.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu Mwenye kubaki limethibiti?
Ibn Baaz: Silitambui.
´Allaamah ar-Raajihiy: Je, lengo la mtunzi linakuwa kwamba anatoa taarifa juu ya Allaah kwa hili?
Jibu: Majina ya Allaah ni kwa mujibu wa dalili ya Qur-aan na Sunnah tu. Hayathibitiki isipokuwa kwa yale yaliyokuja katika Maandiko. Lakini maana yake ni sahihi. Yeye ndiye Aliyebaki daima. Maana yake ni sahihi. Yeye ndiye Aliyebaki daima. Lakini haisemwi kuwa ni miongoni mwa majina Yake ispokuwa kwa kuwepo dalili.
[1] 36:39
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31070/ما-حكم-قول-ان-الله-قديم
Imechapishwa: 01/10/2025
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-kumsifia-allaah-kuwa-ni-wa-kale-na-mwenye-kubaki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket