Ibn Baaz kuhusu kucheza kikoba/kibati

Swali: Ni ipi hukumu ya vikundi vya uchangiaji kati ya wafanyakazi?

Jibu: Vikundi vya uchangiaji vinavyojulikana sasa kwa njia ya mkopo, ambapo wanakusanyika na kila mmoja huchangia kiasi fulani kila mwezi; huyu 1.000, na huyu 1.000, kisha mmoja huchukua 20.000 mwezi huu, mwingine huchukua mwezi mwingine na wa tatu mwezi unaofuata na kadhalika. Hapo awali kulikuwa na shaka na ikakhofiwa kuwa huenda ikawa ni aina ya mkopo unaoleta manufaa. Kisha tukalijadili jambo hili katika baraza la wanazuoni wakubwa na ikatolewa uamuzi kwa rai ya walio wengi kwamba hakuna tatizo katika jambo hili – Allaah akitaka. Ni mkopo usioleta manufaa, bali kila mmoja huchukua sawa na mwenzake, bila ongezeko.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30106/ما-حكم-الجمعيات-التي-تدور-بين-الموظفين
  • Imechapishwa: 11/09/2025