Swali: Ni ipi hukumu ya kubusu msahafu?

Jibu: Hakuna ubaya wowote. ´Ikrimah bin Abiy Jahl, ambaye ni Swahabah, alikuwa akiubusu msahafu. Hata hivyo jambo hilo si lenye kupendeza, kwani halina dalili. Lakini ni sawa ikifanywa kwa nia ya kuitukuza na kuiheshimu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31177/ما-حكم-تقبيل-المصحف
  • Imechapishwa: 10/10/2025