Ibn Baaz kuhusu hukumu ya kifo kwa kunyongwa

Swali: Hivi karibuni imetekelezwa hukumu ya kifo kwa watu watatu nchini Kuwait kwa njia ya kunyongwa. Je, hilo linaafikiana na Shari´ah?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba kinachopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa hukumu ya kifo ni kuchagua njia iliyo nyepesi zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mnapoua, basi afanye uzuri uuaji.”

Kwa mujibu wa yaliyotufikia, kunyongwa si njia nzuri. Kwani kuna mateso ndani yake. Kwa hiyo haipaswi kutumia njia ya kunyongwa, kwa sababu hilo ni kuiga maadui wa Allaah. Bali kinachopaswa ni wauwawe kwa upanga, kwa sababu kuuliwa kwa upanga mikononi mwa mtu mwenye ujuzi na kwa kutumia upanga mzuri kunampa aliyehukumiwa pumziko zaidi na kunamaliza jambo haraka. Hivyo haipaswi kuuliwa kwa njia ya kunyongwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1528/حكم-الاعدام-بالشنق
  • Imechapishwa: 27/03/2026