Ibn Baaz kuhusu Basmalah chooni kabla ya kutawadha

Swali: Kuhusu kumtaja Allaah katika vyoo na sehemu za kujisitiri – je, inakuwa kwa moyo au kwa maneno?

Jibu: Ni kwa moyo.

Swali: Je, kwa maneno ni inachukiza au ni haramu?

Jibu: Inachukiza machukizo ya kujitakasa.

Swali: Vipi kuhusu kutaja jina la Allaah wakati wa wudhuu´?

Jibu: Ikiwa kuna haja ya kufanya wudhuu´ ndani ya choo, ataje jina la Allaah kwa sababu kutaja jina ni wajibu. Asiiache kwa sababu ya machukizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31171/حكم-الذكر-والبسملة-في-الوضوء-عند-الخلاء
  • Imechapishwa: 10/10/2025