Ibn Baaz kuhusu aliyekula vitunguu saumu na vitunguu maji kuja msikitini

Swali: Machukizo ni kwa njia ya machukizo au uharamu?

Jibu: Mtu huyo hatakiwi kuhudhuria. Udhahiri wa makatazo ni uharamu. Haijuzu kwake kuhudhuria hali ya kuwa anayo harufu ya vitunguu saumu na vitunguu maji. Inaruhusiwa kula vitunguu saumu na vitunguu maji. Inafaa kwake kuvila akiwa na hamu navyo. Hata hivyo asihudhurie swalah ya mkusanyiko.

Swali: Je, inakuwa haramu?

Jibu: Hapana, sio haramu. Hata hivyo haijuzu kwake kuhudhuria mkusanyiko mpaka imwondoke ile harufu.

Swali: Kwa nini asihudhurie mkusanyiko?

Jibu: Kwa sababu ya harufu yake inayokera.

Swali: ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mwenye kuvitaka basi avipike.”

Jibu: Anachokusudia avipike.

Swali: Upikaji utaondosha ile harufu mbaya?

Jibu: Utapunguza harufu. Kuhusu vitunguu maji itaondoka ile harufu. Lakini vitunguu saumu pengine harufu isiondoke yote. Lakini akivipika sana pengine navyo harufu ikaondoka au atumie baadhi ya dawa ambazo huondosha harufu hiyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23993/حكم-حضور-من-اكل-الثوم-والكراث-للمسجد
  • Imechapishwa: 09/08/2024