Swali: Je, kufunga baada ya tarehe 15 Sha´baan ni haramu au ni jambo limechukziwa tu?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Sha´baan itapofikia nusu yake basi msifunge.”
Ni Hadiyth Swahiyh. Yule ambaye hakuanza kufunga mwanzoni mwa mwezi basi asifunge baada ya kufika nusu yake kutokana na Hadiyth hii Swahiyh. Vivyo hivyo iwapo atataka kufunga mwishoni mwa mwezi itakuwa ni aula zaidi kutofaa kufanya hivo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja wala siku mbili isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm fulani basi aendelee kuifunga.”
Yule ambaye ana mazowea hakuna neno akaendelea. Kwa mfano mtu ana mazowea ya kufunga jumatatu na alkhamisi ni sawa akaendelea. Kadhalika yule ambaye ana mazowea ya kufunga siku moja na anakula siku ya kufuata ni sawa pia akaendelea. Lakini mtu kuanza kufunga baada ya nusu ya Sha´baan kwa ajili ya Sha´baan haifai.
Ama endapo ataanza kufunga tarehe 14 au tarehe 13 hakuna neno. Ni sawa mtu akafunga mwezi mzima au siku zake nyingi. Lakini mwezi mzima ameanza kula kisha ifikapo katikati yake ndipo anaanza. Hili ndilo lililokatazwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11186/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%8A%D8%A7%D9%85-%D8%A8%D8%B9%D8%AF-%D9%85%D9%86%D8%AA%D8%B5%D9%81-%D8%B4%D8%B9%D8%A8%D8%A7%D9%86
- Imechapishwa: 20/04/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Swawm iliyopendekezwa tarehe 29 na 30 Sha´baan
Swali: Mke wangu anafunga alkhamisi na siku ya jumatatu. Anauliza kama inafaa kwake kufunga kabla ya kuingia mwezi [wa Ramadhaan]? Jibu: Afunge. Hiyo ni ada yake. Ambaye amezowea kufunga swawm fulani afunge. Lakini ambaye alikuwa hana ada ya kufunga asifunge. Nakusudia asifunge tarehe 30 wala tarehe 29 Sha´baan. Asifunge baada…
In "Swawm katika Sha´baan"
Maswali kadhaa kuhusu kuanza kufunga baada ya tarehe 15 Sha´baan
Swali: Vipi kuhusu kufunga swawm inayopendeza baada ya nusu Sha´baan? Jibu: Ikiwa hakuanza kufunga katika ile nusu ya kwanza, basi asifunge nusu iliyobakia. Swali: Nakusudia swawm ya kujitolea yoyote? Jibu: Hapana neno akaendelea kufunga jumatatu na alkhamisi. Ikiwa ana mazowea ya kufunga jumatatu na alkhamisi hapana neno. Swali: Swawm ya…
In "Swawm katika Sha´baan"
Swawm ya siku tatu kwa mwezi na alkhamisi na ijumaa tatu kuangukia siku ya shaka
Swali: Mwenye kufunga mwezi wa Sha´baan aunganishe na Ramadhaan au ni lazima atofautishe kati yake? Kwa mfano mtu ana mazowea ya kufunga siku tatu kila mwezi ambapo swawm yake ikachelewa na akawa amebaki na kesho na kesho yake. Je, anapata dhambi akifunga? Jibu: Hapati dhambi akifunga. Hili linaingia katika maneno…
In "Swawm katika Sha´baan"