Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali wanandoa kuwekeana masharti kabla ya kuoana

Swali: Mwanaume anayo haki ya kwenda na mke wake pale ilipo kazi yake asipomuwekea sharti ya kumbakiza kwa familia yake?

Jibu: Yeye ndiye ana haki naye zaidi. Atakaa naye pale anapotaka na pale wanapokaa wanawake mfano wake. Atabaki kwa familia yake ikiwa ameshurutisha hivo.

Swali: Mwanamke akimuwekea sharti mwanaume kwamba kumuolea juu yake ndio talaka yake. Je, anaachika pale tu atakapooa?

Jibu: Anayo mwanamke huyo sharti yake. Waislamu wako kwa mujibu wa sharti wanazowekeana, kwa sababu kumuolea juu yake kunamdhuru.

Swali: Mwanaume akimuwekea sharti mwanaume kwamba anaweza kumpitia mara moja kwa wiki?

Ibn Baaz: Hadhuriki?

Mwanafunzi: Anadhurika.

Ibn Baaz: Haijuzu. Ni lazima kufanya uadilifu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23855/حكم-اشتراط-المراة-على-زوجها
  • Imechapishwa: 21/05/2024