Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali muhimu kuhusu urefushaji wa swalah ya kupatwa kwa jua

Swali: Je, ni katika Sunnah kutoa mawaidha baada ya swalah ndefu ya kupatwa kwa jua?

Jibu: Hiyo ndio Sunnah. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati lilipopatwa jua aliwaidhi.

Swali: Je, irudiwe tena?

Jibu: Hapana, hairudiwi tena. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuirudia tena. Lakini jua lilichomoza kabla ya kuondoka.

Swali: Je, arefushe kama alivorefusha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Kulingana na hali, awafanyie upole watu. Hali za watu hazivumilii na sio kama hali za Maswahabah. Kwa hivyo kufanywe wepesi baadhi ya mambo.

Swali: Je, watu waswali mpaka lichomoze jua au mwezi?

Jibu: Hapana, kuswaliwe kile kitachowezekana. Waswali Sunnah hata kama halikuchomoza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23884/حكم-الموعظة-والتطويل-في-صلاة-الكسوف
  • Imechapishwa: 27/05/2024