Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali kuhusu ridhaa ya mwanamke mtumzima anapoolewa

Swali: Akimweleza mtumzima ambaye kishaolewa na akanyamaza?

Jibu: Haitoshi. Ni lazima kupata idhini yake wazi isipokuwa msichana bikira. Msichana bikira anastahi na hivyo inatosha akinyamaza. Hata hivyo mwanamke mtumzima ni lazima kumtaka ushauri.

Swali: Je, ndoa ifungwe upya akiridhia baada ya kufungwa ndoa?

Jibu: Ndio, ifungwe upya.

Swali: Akimjamii ilihali ni mwenye kuchukia?

Jibu: Ndoa ifutwe. Baadaye akirdhia ifungwe upya. Hapo ni pale ambapo ataridhia baada ya hapo.

Swali: Mahari atapewa mengine au yatatosha yale mahari aliyopewa mara ya kwanza?

Jibu: Mahari ya kwanza ni kwa kile alichohalalishiwa katika tupu yake mke. Kwa hivyo ni lazima kutolewe mahari mengine ijapo ni kidogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23842/هل-يصح-سكوت-غير-البكر-للاذن-بالنكاح
  • Imechapishwa: 18/05/2024