Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali kuhusu mume kumletea mke dada wa kazi

Swali: Ikiwa mwanamke anasema kuwa yeye hana dada wa kazi na kwamba ni lazima aletewe dada wa kazi. Je, mume wake analazimika kumletea dada wa kazi?

Jibu: Kulingana na mila. Ikiwa wanawake mfano wake wanahudumiwa basi atahudumiwa. Na ikiwa wanawake mfano wake hawahudumiwi basi hatohudumiwa. Kwa maana ya kwamba haimlazimu mume. Lakini hapana vibaya mume akijitolea na akamruhusu. Watu wanatofautiana na miji pia inatofautiana.

Swali: Vipi ikiwa ikiwa wanawake mfano wake hawahudumiwi?

Jibu: Hapo haitomlazimu kumletea dada wa kazi.

Swali: Atalazimika kumhudumia mume wake?

Jibu: Atalazimika kumhudumia ikiwa wanawake mfano wake wanahudumia.

Swali: Vipi ikiwa atang´ang´ania?

Jibu: Wapatane. Wakikujia fanya suluhu baina yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23910/حكم-الزام-الزوجة-لزوجها-بخادم-لها
  • Imechapishwa: 31/05/2024