Swali: Je, Khawaarij ni makafiri?
Jibu: Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba ni waasi. Lakini maoni ya kuwakufurisha ndiyo dhahiri zaidi kwa mujibu wa dalili, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwahusu:
“Wanatoka katika Uislamu kisha hawarudii.”
Kwa hiyo dhahiri ya Sunnah ni kuwa wao ni makafiri. Hao ndio wanaowakufurisha Maswahabah, kuwatia kwenye ufuska na kuwakufurisha wenye madhambi makubwa huku wakiamini kuwa watadumu Motoni milele. Hizi ni imani mbovu na batili. Maoni ya wanaosema kuwa ni makafiri ndiyo yenye nguvu zaidi.
Swali: Je, Ibaadhiyyah wako katika hali ileile ya Khawaarij wa zamani?
Jibu: Wao ni mabaki ya Khawaarij, lakini hawajioneshi waziwazi katika kuwakufurisha Maswahabah. Hata hivyo wanasema kwamba watenda madhambi watadumu Motoni, kama wanavyoamini Khawaarij na Mu´tazilah. Kwa hali yoyote wako katika ´Aqiydah ya Khawaarij na Mu´tazilah kuhusu kudumu watenda madhambi Motoni, japokuwa hawawezi kutamka moja kwa moja kumkufurisha mtenda madhambi. Aidha wanakanusha kumuona Allaah siku ya Qiyaamah na ndani ya Pepo. ´Aqiydah yao ni mbaya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31050/هل-الخوارج-والاباضية-كفار
- Imechapishwa: 30/09/2025
Swali: Je, Khawaarij ni makafiri?
Jibu: Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba ni waasi. Lakini maoni ya kuwakufurisha ndiyo dhahiri zaidi kwa mujibu wa dalili, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwahusu:
“Wanatoka katika Uislamu kisha hawarudii.”
Kwa hiyo dhahiri ya Sunnah ni kuwa wao ni makafiri. Hao ndio wanaowakufurisha Maswahabah, kuwatia kwenye ufuska na kuwakufurisha wenye madhambi makubwa huku wakiamini kuwa watadumu Motoni milele. Hizi ni imani mbovu na batili. Maoni ya wanaosema kuwa ni makafiri ndiyo yenye nguvu zaidi.
Swali: Je, Ibaadhiyyah wako katika hali ileile ya Khawaarij wa zamani?
Jibu: Wao ni mabaki ya Khawaarij, lakini hawajioneshi waziwazi katika kuwakufurisha Maswahabah. Hata hivyo wanasema kwamba watenda madhambi watadumu Motoni, kama wanavyoamini Khawaarij na Mu´tazilah. Kwa hali yoyote wako katika ´Aqiydah ya Khawaarij na Mu´tazilah kuhusu kudumu watenda madhambi Motoni, japokuwa hawawezi kutamka moja kwa moja kumkufurisha mtenda madhambi. Aidha wanakanusha kumuona Allaah siku ya Qiyaamah na ndani ya Pepo. ´Aqiydah yao ni mbaya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31050/هل-الخوارج-والاباضية-كفار
Imechapishwa: 30/09/2025
https://firqatunnajia.com/ibaadhiyyah-ni-mabaki-ya-khawaarij/