Swali: Je, mtu ambaye amepoteza fahamu na aliyezimia wanalazimika kufanya ´ibaadah?
Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemuwajibishia mtu kufanya ´ibaadah pale ambapo anastahiki uwajibu wake, kwa njia ya kwamba awe mwenye akili anayeyafahamu mambo. Kuhusu ambaye hana akili mambo ya Shari´ah hayamlazimu. Kwa ajili hii ´ibaadah haziwalazimu wendawazimu wala watoto ambao hawajabaleghe, jambo ambalo linajulisha rehema Zake Allaah (Ta´ala). Hukumu hiyohiyo inamuhusu mwenye ugonjwa wa akili na mtumzima aliyepoteza fahamu; watu hawa hawawajibiki kuswali wala kufunga. Kwa sababu wako ni kama watoto wadogo wasiokuwa na uwezo wa kupambanua mambo, ikiwa na maana kwamba hawawajibiki kufanya mambo ya ´ibaadah.
Kuhusu mambo ya wajibu ya kimali, wanalazimika kutoa hata kama wameshatokwa na akili. Kwa mfano ni wajibu kwake kutoa zakaah katika mali yake. Ni wajibu kwa yule ambaye anamsimamia kumtolea zakaah kwa niaba yake. Kwa sababu uwajibu wa zakaah umefungamana na mali. Allaah (Ta´ala) amesema:
خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً
“Chukua katika mali zao zakaah.”[1]
Amesema “chukua kutoka katika mali zao” na hakusema achukue kutoka kwao. Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Mu´aadh wakati alipomtuma kwenda Yemen:
“Wakikutii katika hayo, basi wafunze ya kwamba Allaah amewawajibishia kuto zakaah ambayo itachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewa mafukara wao.”
Kujengea juu ya haya ni kwamba yale mambo ya wajibu ya mali hayadondoki kutoka kwa mtu aliyeondokwa na akili. Kuhusu ´ibaadah za kimwili, kama vile swalah, twahara na swawm, yanadondoka kwa sababu hana akili.
Kuhusu ambaye imemwondoka akili yake kwa sababu ya kuzimia kutokana na maradhi na mfano wake, hawajibiki kuswali kwa mujibu wa maoni ya wanzuoni wengi. Mgonjwa akipoteza akili kwa muda wa siku moja-mbili, hahitaji kuzilipa swalah zake kwa sababu hana akili. Halinganishwi na mwenye kulala, ambaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:
“Yule mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[2]
Tofauti ni kwamba mwenye kulala bado yuko na fahamu kwa maana ya kwamba anaweza kuamka atapoamshwa. Hilo ni tofauti na yule aliyezimia. Hapa ni pale ambapo mtu amezimia pasi na sababu. Lakini ikiwa kuzimia ni kutokana na sababu amejisababishia mwenyewe, kama yule ambaye amezimia kutokana madawa ya kulevya na mfano wake, huyu atatakiwa kuzilipa zile swalah zilizompita katika hali ya kutokwa na fahamu – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] 09:103
[2] al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/15-16)
- Imechapishwa: 23/03/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/15-16)
Imechapishwa: 23/03/2026
https://firqatunnajia.com/ibaadah-wakati-wa-kupoteza-fahamu-na-wakati-wa-kuzimia/