Huyu ndiye muumini mwenye nguvu aliyekusudiwa II

Swali: Ni nini makusudio ya Hadiyth isemayo:

”Muumini mwenye nguvu ni bora na mwenye kupendwa zaidi na Allaah kuliko muumini dhaifu.”?[1]

Kuna wanaosema kuwa makusudio ya nguvu ni za mwili.

Jibu: Hapana, haikusudiwi nguvu ya mwili pekee. Nguvu inayokusudiwa hapa ni nguvu ya matendo. Akiwa na nguvu zaidi ya ndovu, lakini haamrishi mema wala hakatazi maovu, basi hawezi kuitwa kuwa ni mwenye nguvu; badala yake anakuwa ni dhaifu, hata kama ana nguvu zaidi kuliko ndovu.

[1] Muslim (04/2052).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25244/ما-المقصود-بحديث-المومن-القوي-خير-واحب-الى-الله
  • Imechapishwa: 20/02/2025