Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

127 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لَقدْ رَأيْتُ رَجُلًا يَتَقَلَّبُ في الجَنَّةِ في شَجَرَةٍ قَطَعَهَا مِنْ ظَهْرِ الطَرِيقِ كَانَتْ تُؤذِي المُسْلِمِينَ

“Nilimuona mtu akitembea Peponi kwa sababu ya mti alioukata njiani uliokuwa ukiwaudhi waislamu.”[1]

Katika Hadiyth hii kuna dalili inayoonyesha kuwa yule atayemwondoshea matatizo ndugu yake muislamu ana ujira mkubwa juu ya kitu cha kihisia. Tusemeje juu ya kitu cha kimaana?

Kuna baadhi ya watu – Allaah atukinge – ambao ni watu wa shari na maovu, fikira chafu na tabia mbaya wanawazuia watu na dini ya Allaah. Kuwaondosha watu hawa katika njia ya waislamu ni bora zaidi na jambo lenye ujira mkubwa mbele ya Allaah (´Azza wa Jall). Ikiwa ni watu wenye fikira chafu na za kikafiri, mtu aondoshe shari yao kwa kuwaraddi na kubatilisha fikira zao. Ikiwa shari yao haikutokomea kwa njia hiyo, wauawe[2]. Kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) anasema katika Kitabu Chake kitukufu:

إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ

“Hakika hapana vyengine malipo ya wale wanaompiga vita Allaah na Mtume Wake na wakaeneza maharibifu katika ardhi, wauawe au wasulubiwe au ikatwe mikono yao na miguu kinyumenyume au watolewe katika nchi.”[3]

[1]Muslim (1914).

[2] Zayd al-Madkhaliy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Si haki ya kila mmoja kusimamisha adhabu za Kishari´ah. Isipokuwa yule aliyetawalia madaraka ya waislamu. Mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye haki ya kusimamisha adhabu kama vile ya kumuua anayeua makusudi, anakata mkono wa mwizi, anampiga bakora mzinzi ambaye hajawahi kuingia ndani ya ndoa, atampiga mawe mzinzi ambaye kishawahi kuingia ndani ya ndoa na atampiga mijeledi mtu ambaye anawatuhumu wengine machafu na mnywaji pombe. Wakati mwingine adhabu inaweza kuwa kwa njia ya kuua. Yote haya ni mambo yanayopasa mamlaka. Hakuna mwengine yeyote, hata kama ni mwanachuoni,  anayo haki ya kusimamisha adhabu si juu ya nafsi yake mwenyewe wala waja wengine isipokuwa ikiwa kama ana idhini kutoka kwa mtawala, kwa mfano mahakimu wa kidini na maafisa wa polisi. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya jambo hili.” (at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 17-18)

[3] 05:33

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/175-176)
  • Imechapishwa: 04/06/2024