Hukumu ya wale wenye kubusa na kupapasa ukuta al-Madiynah

Swali: Katika mji wa al-Madiynah wapo baadhi ya watu ambao wanalibusu kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanamnyooshea mkono na wanamuomba. Je, inafaa kwetu kuwajengea dhana njema kwamba wanajiombea wenyewe?

Jibu: Huu ni ujinga. Wanatakiwa kufunzwa na kuelezwa kwamba wanapotaka kuomba wanatakiwa kuelekea Qiblah au waende sehemu nyingine ili wasije kujishawishi wenyewe au wakawashawishi wengine ambapo wakawafikiria kuwa wanamuomba Mutme (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 34
  • Imechapishwa: 13/06/2019