Hukumu ya minara juu ya misikiti

Swali: Vipi kuhusu aliyesema kwamba minara iliyoko misikitini ni katika mambo ya Bid´ah iliyozuliwa?

Jibu: Hapana, maneno hayo si sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamuru adhaana itolewe sehemu za juu, kama vile juu ya paa au sehemu nyingine, kwa sababu lengo ni kuwafikishia watu sauti. Kadiri sehemu inavyokuwa ya juu zaidi, ndivyo inavyowafikia watu wengi zaidi.

Swali: Kuhusu mimbari, wanasema kuwa ikiwa ina zaidi ya ngazi tatu ni Bid´ah?

Jibu: Jambo hilo ni pana kwa idhini ya Allaah, jambo hilo ni lenye wasaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31552/ما-حكم-المنارات-والمنابر-في-المساجد
  • Imechapishwa: 02/11/2025