Hukumu ya mchezo wa karata

Swali: Mara nyingi tunacheza karata na watu wenye pesa nyingi na yule mshindi tunampa kila mmoja pesa 200. Je, kufanya hivo ni haramu na kamari?

Jibu: Mchezo huu kwa sura iliyotajwa ni haramu. Ni kamari. Kamari ndio ile (الميسر) iliyotajwa katika maneno Yake (Subhaanah):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ

“Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na kuabudu masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli ni uchafu kutokana na kazi ya shaytwaan, hivyo basi jiepusheni navyo mpate kufaulu. Hakika si venginevyo shaytwaan anachotaka kukutilieni kati yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na swalah, basi, je, mtakoma?”[1]

Kwa hivyo ni lazima kwa kila muislamu kumcha Allaah na atahadhari juu ya mchezo huu na miengineyo katika aina za kamari ili aweze kufuzu na apate mwisho mwema. Jengine pia ni kwamba apate kusalimika na zile shari nyingi zilizotajwa katika Aayah mbili zinazotokana na mchezo huu.

[1] 05:90-91

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/489)
  • Imechapishwa: 28/05/2021