Hukumu ya manjano na uchafu mwepesi ulioambatana na hedhi

Swali: Vipi kuhusu rangi ya manjano na uchafu mwepesi iwapo vimeambatana na hedhi, kuanzia mwanzo wa hedhi ikawa ni manjano na uchafu mwepesi?

Jibu: Hali ni hiyohiyo – ikiwa mwanzo wa hedhi ni manjano na uchafu mwepesi, mwisho wake ni manjano na uchafu mwepesi, basi inahesabiwa kuwa ni sehemu ya hedhi ya kawaida.

Swali: Vipi ikiwa damu inamjia baada ya hiyo manjano na uchafu mwepesi?

Swali: Ikiwa imeambatana, basi inakuwa ni sehemu ya hedhi yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia mwanamke mwenye damu ya ugonjwa:

“Kaa kwa muda ambao hedhi yako ilikuwa inakuzuia kisha oga.”

Na kila aliyemwendea akilalamikia hali hiyo alimwambia:

“Kaa kwa muda ambao hedhi yako ilikuwa inakuzuia kisha oga.

Hiki ndio kigezo cha kutokea. Baadhi ya wanawake hali yao huwa imenyooka, hata kama siku zake za mwisho zitaongezeka siku au mbili, hili linatokea kwa wanawake. Hivyo wasiwe na haraka mpaka waone wamesafika.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27525/حكم-الصفرة-والكدرة-اذا-اتصلت-بالعادة
  • Imechapishwa: 11/04/2025