Hukumu ya majimaji yanayomtoka mtu wakati wa kukojoa

Swali: Mimi tangu nitoke safarini ni mwenye kudumu kuswali na hivi sasa nina miaka kumi na tisa. Wakati ninapojisafisha kutokamana na mkojo huona majimaji yenye kutoka yanayofanana na manii. Je, majimaji haya yanawajibisha kuoga?

Jibu: Majimaji haya hayawajibishi kuoga. Kwa sababu sio manii. Ni majimaji yanayotoka wakati wa kukojoa. Manii yanayowajibisha kuoga ni yale yanayomtoka mtu kwa matamanio. Haya ndio manii yanayowajibisha kuoga. Kuhusu majimaji yanayotoka pasi na matamanio hayawajibishi kuoga. Isipokuwa ikiwa yamemtoka mwenye kulala. Mwenye kulala akiamka kutoka usingizini mwake na akaona athari ya manii ni lazima kwake kuoga. Ni mamoja amekumbuka kuwa ameota au hakukumbuka. Ama ambaye yuko macho si lazima kwake kuoga kwa kutokwa na manii isipokuwa yakimtoka kwa matamanio.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (11) http://binothaimeen.net/content/6753
  • Imechapishwa: 05/12/2020