Hukumu ya maamuma kutangulia mbele ya imamu katika swalah

Swali: Wako watu wanaoswali katika msikiti mtukufu wa al-Madiynah na wanatangulia mbele ya imamu. Ni ipi hukumu ya hilo? Swalah ni sahihi au hapana?

Jibu: Masuala haya yana tofauti kati ya wanachuoni. Wako ambao wameonelea kuwa inasihi wakati wa dharurah. Wako wengine ambao wanaonelea haisihi kabisa. Vile ambavo naona ni kwamba wasitangulie mbele. Yule ambaye ameswali mbele ya imamu basi kinachompasa ni yeye kuirudi. Kwa sababu maoni yanayosema kuwa swalah yake haisihi ni maoni yenye nguvu. Haitambuliki kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah zake kuswali mbele ya imamu. Ni kitu kinachoenda kinyume na msimamo wa Kishari´ah. Madai ya kwamba ni dharurah haitakiwi kwa mtu kujisalimisha kwayo. Kwa sababu hakuna dharurah kwa wewe kuswali mbele ya imamu. Msipopata sehemu basi swalini nyumbani kwenu au katika msikiti mwingine ukiweko. Ama kusema mtu atangulie mbele ya imamu hakuna dharurah hiyo. Lililo la wajibu ni kufuata Shari´ah; ima mtu awe upande wa kulia mwa imamu, upande wa kushoto au nyuma yake. Ama kusema kumtangulia mbele ni jambo linakwenda kinyume na msimamo wa Kishari´ah. Ambaye ameswali mbele ya imamu kinachompasa ni yeye airudi kwa ajili ya kutendea kazi maoni ya ambaye amekataza hilo. Kwani ndio jambo linaloafikiana na uinje wa dalili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4779/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D9%82%D8%AF%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%A7%D9%85%D9%88%D9%85-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%85%D8%A7%D9%85-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 02/10/2020