Hukumu ya kutufu na kukhitimisha Qur-aan kwa ajili ya wafu


Swali: Baadhi ya nyakati namfanyia Twawaaf mmoja katika ndugu zangu, baba yangu au babu yangu ambaye kishafariki. Ni ipi hukumu ya hilo? Ni ipi hukumu ya kuwakhitimishia Qur-aan?

Jibu: Bora ni kuacha kufanya hivo kwa kutokuwa na dalili ya jambo hilo. Lakini imewekwa katika Shari´ah kumtolea swadaqah yule umtakaye katika ndugu zako au wengieno wakiwa ni waislamu, kuwaombea du´aa na kuwafanyia hajj na ´umrah.

Kuhusu kuswali kwa ajili yao, kuwafanyia Twawaaf na kuwasomea Qur-aan bora ni kutofanya hayo kwa kutokuwa na dalili ya mambo hayo. Baadhi ya wanachuoni wameyajuzisha mambo hayo kwa kutumia Qiyaas juu ya swadaqah na kuwaombea du´aa. Lakini lililo salama zaidi ni kuacha kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/900/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B7%D9%88%D8%A7%D9%81-%D9%88%D8%AE%D8%AA%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%B1%D8%A7%D9%86-%D9%84%D9%84%D8%A7%D9%85%D9%88%D8%A7%D8%AA
  • Imechapishwa: 04/12/2019