Swali: Inajuzu kwa mswaliji kutawadha bila ya kuosha miguu yake na akapangusa juu ya viatu?

Jibu: Wakati wa kutawadha ni lazima kwa mtu kuosha uso wake – ndani yake kunaingia kusukutua na kupandisha maji puani – akaosha mikono yake kuanzia kwenye ncha za vidole hadi kwenye kisugudi, kufuta kichwa chake chote – ndani yake kunaingia pia masikio – na akaosha miguu yake. Twahara isipotimia kwa njia hii basi si sahihi na wala haisihi kwa mtu kuswali nayo.

Kuhusu kufuta juu ya viatu haijuzu. Ni lazima kuvua viatu na kuosha mguu.

Kuhusu khofu/soksi inafaa kufuta juu yake. Ni lazima khofu hizo ni za ngozi, pamba au kitu kingine. Kwa sharti iwe katika vile vitu ambavo ni halali kuvivaa. Ama ikiwa ni katika vitu ambavyo ni haramu kuvivaa, kama mfano wa hariri kwa mwanaume, kama akivaa soksi za hariri haitofaa kwake kufuta juu yake kwa sababu ni haramu kwake kuivaa. Ikiwa ni kitu kilichoruhusiwa itafaa kufuta juu yake midhali mtu alizivaa akiwa na wudhuu´ na iwe ndani ya ule muda uliopangwa na Shari´ah ambapo ni mchana na usiku mmoja kwa mkazi na michana mitatu na nyusiku zake kwa msafiri. Muda huu unaanza kuhesabiwa kuanzia pale mara ya kwanza atapoanza kupangusa na unaisha kwa kumalizika masaa ishirini na nne kwa mkazi na masaa sabini na mbili kwa ambaye ni msafiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (15) http://binothaimeen.net/content/6791
  • Imechapishwa: 05/03/2021