Swali: Baadhi ya watu wazuri wameoa baadhi ya wanawake wachafu au kinyume chake…

Jibu: Hili haliwezekani. Hili haliwezekani – kwa idhini ya Allaah. Wanawake wachafu bi maana wazinifu. Muislamu hawezi kumuoa mwanamke mzinifu:

الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ

“Mwanamme mzinifu hafungi ndoa isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina, na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina.” (24:03)

Wala sio sahihi kumuoa. Isipokuwa akitubu na Zinaa na akatoka katika eda, anaweza kuolewa. Lakini maadamu bado hajatubia na Zinaa, sio sahihi na wala haijuzu kumuoa. Ni ndoa batili.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (65) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13832
  • Imechapishwa: 16/11/2014