Hukumu ya kumsujudia asiyekuwa Allaah

Swali: Vipi kuhusu kusujudia sanamu?

Jibu: Kusujudu kwa sanamu ni ukafiri mkubwa, ni mamoja iwe kwa ajili ya sanamu, aliye ndani ya kaburi, kwa mtawala, kwa Zayd au kwa ´Amr. Kusujudia asiyekuwa Allaah ni ukafiri mkubwa. Allaah amesema:

فَاسْجُدُوا لِلَّـهِ وَاعْبُدُوا

”Basi msujuduni kwa ajili ya Allaah na mwabuduni Yeye.”[1]

Swali: Wako wanaosema kuwa ni lazima uitakidi?

Jibu: Hapana, hapana. Pale tu atapomsujudia asiyekuwa Allaah anakufuru.

Swali: Wamelinganisha na sujuud ya Mu´aadh kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapana, hapana. Sujuud ya Mu´aadh Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwonya kwamba hakuna yeyote anayepaswa kumsujudia mwingine na akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Lau ningemwamrisha mtu kumsujudia yeyote, basi ningemwamrisha mwanamke amsujudie mumewe, kutokana na ukubwa wa haki yake juu yake.”[2]

Kuhusu sujuud ya ndugu zake Yuusuf, hilo lilikuwa katika Shari´ah ya waliokuwa kabla yetu. Kwao wao ilikuwa ni sujuud ya mamkizi. Kadhalika sujuud ya Malaika kwa Aadam ni sujuud ya heshima na mamkizi. Hilo ni jambo maalum. Inapokuja katika Shari´ah hakuna jambo la kumsujudia yeyote asiyekuwa Allaah:

فَاسْجُدُوا لِلَّـهِ وَاعْبُدُوا

”Basi msujuduni kwa ajili ya Allaah na mwabuduni Yeye.”

[1] 53:62

[2] at-Tirmidhiy (1159).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29286/حكم-السجود-لغير-الله-تعالى
  • Imechapishwa: 04/09/2025