Hukumu ya kukesha usiku na kuchelewesha Fajr

Swali: Tunamshtakia Allaah kisha wewe ya kwamba vijana wengi hatuwaoni wakiswali swalah ya Fajr siku hizi. Sababu inawezekana kuwa wanakesha na kulala. Unawanasihi nini? Ni ipi hukumu ya ambaye anaacha swalah ya Fajr mpaka jua likachomoza na hilo likawa kwa kuendelea?

Jibu: Kuhusu nasaha zangu kwa watu hawa udhahiri ni kwamba maneno yangu juu ya hilo ni kwa njia ya kukariri. Kila mmoja anafahamu ya kwamba haijuzu kwa mtu kukesha usiku kisha akaacha swalah ya Fajr.

Ama wale ambao wanachelewesha swalah ya Fajr mpaka ukatoka wakati wake pamoja na kuwa wanaweza kuswali ndani ya wakati, watu hawa hazikubaliwi swalah zao japokuwa wataswali mara elfumoja. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”

Yule anayechelewesha swalah mpaka ukatoka wakati wake bila ya kuwepo sababu ya Kishari´ah, basi hakika huyo amefanya kitendo kisichoafikiana na amri ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hivyo kitakuwa ni chenye kurudishwa kwake mwenyewe. Lakini hata hivyo ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah na akithirishe kufanya matendo mema. Tunamuomba Allaah usalama.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/873
  • Imechapishwa: 06/07/2018