Hukumu ya kufanya kikomo cha uzazi

Swali: Inajuzu kufanya kikomo cha watoto katika maisha ya kindoa?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo. Kilichowekwa katika Shari´ah kwa mtu azae watoto wengi. Lengo ni kuufanya Ummah wa Kiislamu kuwa mkubwa. Kuhakikisha kujifakharisha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Ummah wake. Jengine ni kutokana na ile kheri na manufa yanayopatikana ndani yake. Watoto hawa wanaweza kuwa wema wenye kuwafaa wazazi wao katika dini na dunia yao.

Jengine ni kwamba kufanya kikomo cha watoto si jambo liko mikononi mwa mtu. Mtu anaweza kuweka kikomo cha watoto wane au watano. Kisha baadaye watoto hawa au baadhi yao wakafariki. Matokeo yake akabaki akiwa ni tasa au mwenye watoto wachache.

Kwa hali yoyote kufanya kikomo cha watoto ni jambo halijuzu. Ama kuhusu kupanga kwa maana ya kwamba badala ya mwanamke kuzaa kwa miaka miwili mara mbili na akataka kwa mwaka azae mara moja, kwa ajili ya manufaa ya Kishari´ah, haina neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (06) http://binothaimeen.net/content/6689
  • Imechapishwa: 01/11/2020