Hukumu ya kufanya kikomo cha uzazi

Swali: Vipi kuhusu kuweka kikomo cha uzazi?

Jibu: Haitakikani kuweka kikomo cha kizazi. Isipokuwa ikihitajika na manufaa yakipelekea kufanya hivo kwa muda maalum.

Swali: Makatazo ya kuweka kikomo cha uzazi ni kwa njia ya uharamu?

Jibu: Maoni ya karibu zaidi ni kwa njia ya uharamu, kwa sababu ummah umetakiwa kujitahidi kuufanya mkubwa, kupata kizazi na kujizuia na machafu. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba inachukiza. Lakini udhahiri wa dalili ni makatazo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23893/ما-حكم-تحديد-النسل
  • Imechapishwa: 28/05/2024