Swali: Niliswali na imamu na nilikuwa nimekuja nimechelewa Rak´ah moja. Imamu alipotoa Tasliym nami nikatoa Tasliym hali ya kusahau. Papo hapo baada ya swalah nilipokumbuka nikakamilisha swalah yangu. Lakini sikusujudu sijda ya kusahau. Je, juu yangu kuna kitu?
Jibu: Ikiwa uliacha sijda ya kusahau kwa makusudi, basi swalah yako ni batili. Na ikiwa uliiacha kwa kusahau, basi unatakiwa kusujudu pale utakapokumbuka na hivyo swalah yako ni sahihi. Ingawa baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa kukishapita muda kitambo kirefu au wudhuu´ wako ukachenguka basi sijda [ya kusahau] inadondoka.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
- Imechapishwa: 08/08/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Hukumu ya aliyechelewa ambaye hakumfuata imamu katika sujudu ya kusahau
Swali: Niliswali pamoja na imamu na nilikuwa nimechelewa. Imamu alipotoa Tasliym nikasimama kwa ajili ya kulipa. Tahamaki imamu akasujudu sujudu ya kusahau baada ya Tasliym lakini hata hivyo sikumfuata katika sujudu yake ya kusahau na wala sikusujudu baada ya kumaliza kulipa kwangu. Je, kuna jambo linalonilazimu? Je, nirudi swalah yangu?…
In "Mkusanyiko (Jamaa´ah)"
Ametoa Tasliym kabla ya imamu kwa kusahau
Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anatoa Tasliym kabla ya imamu kwa kusahau? Je, swalah yake ni sahihi? Jibu: Mswaliji akitoa Tasliym kabla ya imamu hali ya kusahau kisha akazindukana, basi arejee katika nia ya swalah. Kisha baada ya hapo atoe Tasliym baada ya imamu wake na wala hakuna kitu…
In "Mkusanyiko (Jamaa´ah)"
Swalah ya ambaye amesujudu sijda moja badala ya mbili
Swali: Imamu ameswali swalah ya ´Aswr na katika Rak´ah ya mwisho akasujudu sijda moja peke yake na akaketi Tashahhud ya mwisho na akatoa Tasliym. Baada ya hapo akazinduliwa na baadhi ya waswaliji kwamba amesujudu sijda moja peke yake na hakusujudu sijda ya pili katika ile Rak´ah ya mwisho. Kisha akasimama…
In "Sujuud"