Hukumu ya jihaad Bosnia na Herzegovina mwaka wa 1992

Swali: Ni ipi hukumu ya jihaad Bosnia na Herzegovina chini ya hali ya sasa na shambulio kali la wakristo walioko kwenye vita dhidi ya waislamu huko ni ipi – kwa ajili ya wabosnia na yale mataifa jirani yalioko Ulaya na kwa ajili ya wakaazi wa nchi za kiarabu na Kiislamu – ikizingatiwa kuwa viongozi wengi wa uwanja huko wanasema wanahitaji silaha na watu, khaswa kutoka waarabu?

Jibu: Waislamu huko wako katika haja kubwa ya msaada wa watu, pesa na silaha katika Bosnia na Herzegovina. Wako katika haja kubwa ya msaada. Jihaad ni wajibu na kuwasaidia ni wajibu kwa watawala wa waislamu na kwa kila mtu. Hata hivyo mara watu fulani wakisimama na jukumu wajibu huo basi inadondoka kutoka kwa wengine, kwa sababu ni faradhi yenye kutosheleza. Hali yao sasa ni ya kusikitisha na maadui wamewazunguza. Wao wanahitaji kwa haraka msaada na kuruhusiwa kununua silaha ili kujilinda dhidi ya adui huyo mhalifu wa Serbia. Tunaomba Allaah awape mafanikio, awanusuru dhidi ya adui zao na awatokomeze maadui wa Uislamu na awafungie mduara.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30972/ما-حكم-الجهاد-في-البوسنة-والهرسك
  • Imechapishwa: 22/09/2025