Swali: Tumesikia kutoka kwako fatwa kuhusu kukhitimisha. Je, inahusiana na du´aa ya kukhitim au ni kukhitimisha msahafu?
Jibu: Sijui anachomaanisha. Kitu kilicho na nguvu kilichopokelewa kuhusu kukhitimisha ni yale yaliypokelewa kutoka kwa Anas (Radhiy Allaahu ´anh) ya kwamba pale anapotaka kukhitimisha Qur-aan anaikusanya familia yake kisha anaomba nyumbani kwake. Inahusiana na familia yake tu. Kuhusu ndani ya swalah sijasikia hilo, si kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa yeyote kutoka kwa Maswahabah, lakini hata hivyo wamelipendezesha baadhi ya wanachuoni. Kwa hivyo ni jambo lina tofauti. Ikishakuwa mambo ni hivo kwamba kuna wanachuoni wamelipendezesha na yule imamu tunayeswali nyuma yake anaonelea hivo, tunatakiwa kumfuata. Ama mtu kukwepa mkusanyiko wa msikitini ni kosa. Midhali mambo haya wanachuoni wametofautiana na mimi nipo basi haitakiwi kutofautiana na watu. Hali imefikia kiasi cha kwamba mpaka Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah), pamoja na pupa yake katika Sunnah na kuifuata, amesema: “Mtu akiongozwa na mtu mwenye kukunuti katika swalah ya Fajr basi amfuate na aitikie “Aamiyn” juu ya du´aa yake.” Imaam Ahmad anaonelea kuwa hakuna Qunuut katika swalah ya Fajr na haikusuniwa. Lakini pamoja na hivyo anaonelea ukiswali nyuma ya imamu ambaye anasoma Qunuut mfuate na uitikie “Aamiyn” juu ya du´aa yake. Yote haya ili mtu asitofautiane na mkusanyiko. Umoja siku zote ni kheri. Lau vijana wetu wangelijali suala hili la umoja na wakapuuzilia mbali yale yote yanayopelekea katika tofauti ingelikuwa ni kheri kubwa. Lakini vijana wengi imekuwa pale anapomuona nduguye ameshika mwelekeo usiokuwa wake basi anamfanyia uadui kwa ajili hiyo, anamzungumza kwenye vikao na anatahadharisha naye. Hili ni kosa kubwa. Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu. Watu wema ambao wanapenda kheri na ambao mwelekeo wao ni wa sawa ndio ambao wanapeana majina bandia na ndio ambao wanatofautiana na upande mwingine watu wa shari neno lao ni moja. Nii ni aibu kwa watu wa kheri.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1617
- Imechapishwa: 03/10/2018

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1617
Imechapishwa: 03/10/2018
https://firqatunnajia.com/hukumu-ya-duaa-ya-kukhitimu-msahafu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)