Hukumu ya anayeokota kitu chini kilichomwanguka wakati wa swalah

Swali: Kuna mtu alikuwa anaswali Dhuhr ikamuanguka leso ambapo alikuwa amesimama akainama na kuikota. Je, swalah yake inabatilika kwa kutikisika namna hii?

Jibu: Ndio, swalah yake inabatilika kwa kutikisika namna hii. Kwa sababu atapoinama itamuhitajia yeye kwenda chini mpaka afike kwenye Rukuu´ na kwa njia hiyo atakuwa amezidisha Rukuu´. Lakini akiwa ni mjinga hana juu yake kitu. Kutokana na ujumla wa maneno Yake (Ta´ala):

 رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee wetu! Usituchukulie pale tunaposahau au kukosea.”  (2:286)

Kwa hivyo ukiponyokwa na leso au funguo ilihali umesimama waswali, iache mpaka pale utapoenda katika Sujuud. Vilevile unaweza kuichukua kwa mguu wako. Ikiwa unaweza kubaki unasimama kwa mguu mmoja, basi chukua kwa mguu wako na uikamate kwa mkono wako. Ama mtu kuinama kutoka chini kwenye ardhi uinamaji ambao utakufanya uwe kwa namna ya kuruku kuliko kusimama ni jambo lisilojuzu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/837
  • Imechapishwa: 30/07/2018