Hukumu ya anayeapa vile inavyompelekea dhana yake kubwa

Swali: Akiapa huku akiwa na dhana kubwa ya kuwa jambo fulani limetokea, lakini halijatokea. Je, atalazimika kutoa kafara?

Ibn Baaz: Kwa maana ya kwamba ameapa kwamba jambo hilo limetokea?

Muulizaji: Ameapa kwamba jambo fulani limetokea, lakini halijatokea.

Ibn Baaz: Amesahau?

Mwanafunzi: Dhana kubwa imempelekea kufanya hivo.

Ibn Baaz: Naapa kwamba fulani amekuja, naapa kwamba fulani amefika na naapa kwamba mwezi umeshaingia. Akifikiri hivo?

Mwanafunzi: Ndiyo.

Jibu: Sahihi ni kwamba hakuna juu yake kafara, kwa sababu anajiona ni mwenye kusema ukweli.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28966/حكم-من-حلف-على-شيء-بغلبة-ظنه
  • Imechapishwa: 14/05/2025